Kampuni ya GSM imemzawadia Tsh Milioni 5 kijana Majaliwa Jackson ambaye aliokoa watu 24 kwenye ajali ya ndege iliyoanguka ziwani mkoani Kagera
Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara, amebainisha kuwa Mwenyekiti wa GSM Foundation, Ghalib Said Mohamed (GSM), ambaye taasisi yake imekuwa ikijihusisha na masuala ya kijamii, ameagiza Majaliwa apewe tunzo hiyo
Kijana huyo pia alizawadiwa Tsh Milioni 1 na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kagera huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiagiza Majaliwa apewe ajira katika jeshi la Uokozi

ADVERTISE HERE