Nsajigwa asisitiza ushindi utapatikana Shelisheli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2018
Nsajigwa asisitiza ushindi utapatikana Shelisheli
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema wamejiandaa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya St Louis keshokutwa.

Akizungumza jana muda mfupi kabla ya Yanga haijakwea pipa kwenda Shelisheli, Nsajigwa alisema licha ya kupata ushindi 'kiduchu' wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza, wamebaini makosa yaliyowanyima ushindi mnono kwenye mchezo wa kwanza.

"Hatutacheza soka la kuzuia kwa muda wote, mchezo uliopita sisi kama benchi la ufundi tumeona mapungufu yao na nini tulitakiwa kukifanyia kazi, na tumefanya hivyo," alisema Nsajigwa.

"Mahesabu yetu tunataka kupata bao la mapema ili kuwachanganya na sisi kujiweka katika nafasi nzuri kwa kuuteka mchezo.

"Nikiri tu hautakuwa mchezo rahisi, lakini tunaenda kupambana kwa sababu tuna mbinu za kutuwezesha kufanya hivyo," aliongeza kusema Nsajigwa.

Kwenye mchezo huo Yanga itamkosa kinara wake wa mabao Obrey Chirwa aliyebaki jijini Dar es salaam akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.

Kiungo Papi Tshishimbi na mshambuliaji Ibrahim Ajib wamepewa jukumu na benchi la ufundi kuhakikisha Yanga inasonga mbele.

Wengine ni Emanuel Martin ambaye yuko katika kiwango bora sambamba na Pius Buswita.

Yanga imesafiri na wachezaji 20.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’