Wale waarabu Club Africain hawatakaa wamsahau Salum Abubakar 'Sure Boy' kwa alichowafanya jana katika uwanja wao wa Hammadi Agrebi Olympic Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho kwa mara ya tatu katika historia yao. Yanga pia ilicheza makundi ya michuano hiyo mwaka 2016 na 2018
Krosi yake kutoka upande wa kushoto kwenye dakika ya 79 ilitua kichwani kwa Fiston Mayele aliyemtengea Stephane Aziz Ki aliyeweka kimiani bao pekee la ushindi lililoipeleka Yanga makundi
Hakuna shaka, Sure Boy alikuwa nyota wa mchezo huo, alitawala eneo la kiungo, kwa hakika ilikuwa sapraizi kubwa kutoka kwa kocha Nasreddine Nabi
Hakucheza mechi ya kwanza iliyopigwa jijini Dar es salaam hivyo Club African hawakuwa na taarifa zake
Wachezaji wote wa Yanga walipambana kwelikweli siku ya jana lakini Sure Boy na mlinda lango Djigui Diarra walikuwa 'wa moto' hasa
Huyu Sure Boy lazima atawatokea sana usingizini Club Africain, haishangazi baada ya mechi walichafukwa na wakawafanyia vurugu wachezaji wa Yanga