Wale waliosema Nabi hafai mnawasikia huko?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Nov 2022
Wale waliosema Nabi hafai mnawasikia huko?

Wakati mwingine ni vyema sisi mashabiki tuupende mpira kwanza kabla ya mapenzi ya timu zetu

Kwa sababu kama unapenda timu zaidi kuliko mpira wenyewe, zipo nyakati timu yako itakosa matokeo mazuri na utakuwa kwenye wakati mgumu

Duniani hakuna timu ambayo itafanya vizuri katika kila mchezo zipo nyakati za kuanguka na kujipanga upya

Tuliona presha ambayo ilitengezwa dhidi ya Kocha Nasreddine Nabi baada ya matokeo ya mchezo wa kwanza dhidi ya Club Africain uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Wapo wengine walikwenda mbali na kushinikiza Nabi aondolewe eti kwa kuwa ametoka suluhu ya bila kufungana na Club Africain

Wakasahau kuwa Nabi huyu huyu ndiye aliyeirejesha furaha Wananchi baada ya misimu minne ya mateso

Ni Nabi huyu huyu ambaye timu yake imecheza mechi 45 mfululizo katika ligi kuu pasipo kupoteza

Jana amewadhihirishia ni kwa kiasi gani ni kocha bora ambae kwa hakika kama viongozi wa Yanga wangeingia mtegoni wakati ule wa presha ya mashabiki, pengine wangejilaumu

Kila mmoja anaipongeza Yanga kwa kucheza vizuri dhidi ya Club Africain hapo jana na kupata ushindi wa bao 1-0

Lakini aliyetengeneza mpango mkakati wa mechi ile ni Nabi, alijua vijana wake wanahitaji kucheza vipi ugenini dhidi ya timu ngumu na hatimaye ushindi ukapatikana

Yanga imeingia makundi Shirikisho, huu unaweza kuwa msimu bora sana kwa Yanga katika michuano hiyo chini ya Nabi

Mwaka 2016 (Hans van Pluijm) na 2018 (Lwandamina/Zahera) Yanga ilicheza makundi ya Shirikisho na ilimaliza katika nafasi ya mwisho

Chini ya Nabi msimu huu Yanga itafanya zaidi ya kile walichofanya katika michuano hiyo miaka iliyopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’