Msafara wa kikosi cha Yanga uliondoka Tunisia jana na leo majira ya mchana wanatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
Msafara ulitua Dubai majira ya usiku ambapo wamelala hapo na leo asubuhi majira ya saa tatu wataianza safari kurejea Tanzania
Wakiwasili Tanzania, wachezaji watakuwa na mapumziko ya muda mfupi kabla ya kuunganisha kuelekea jijini Mwanza ambako wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar keshokutwa Jumapili katika uwanja wa CCM Kirumba




ADVERTISE HERE