Baada ya kurejea nchini kutoka Tunisia, Wachezaji na benchi la ufundi la Yanga walipata mapumziko ya muda mfupi kisha majira ya saa tatu usiku walikwea pipa kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa CCM Kirumba. Kumekuwa na maoni na malalamiko kuhusu ratiba hii ya kucheza mechi mfululizo lakini hakuna namna, Bodi ya Ligi imesisitiza hakuna viporo
Pamoja na uchovu Wananchi wako Mwanza na kesho watashuka CCM Kirumba kuzisaka alama tatu




ADVERTISE HERE