Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ameruhusiwa kwenda kutekeleza majukumu ya timu ya Taifa ya Burkina Faso
Aziz Ki hakurejea na wachezaji wengine wa Yanga jana akipewa ruhusu kujiunga na timu ya Taifa
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wamemruhusu Aziz Ki kwenda kujiunga na timu ya Taifa kwa kuwa kwa sasa hawezi kuichezea Yanga akiwa amefungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi
"Ni kweli Aziz Ki atakosekana. Amefungiwa na Bodi ya Ligi na sisi benchi la ufundi tumemruhusu akajiunge na kambi yake ya timu ya Taifa. Tunaamini huko atakuwa kwenye maandalizi mazuri ya kucheza na atarudi akiwa imara sana," alisema Kaze
Yanga iko mkoani Mwanza ambapo kesho Jumapili itashuka uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC