Mshambuliaji wa Yanga kinara wa mabao Obrey Chirwa amekerwa na uzushi unaoenezwa na baadhi ya magazeti na kwenye mitandao ya kijamii kuwa ameitaka klabu ya Yanga imlipe Mil 150 ili aweze kusaini mkataba mpya.
Chirwa amedai anatambua kuna watu wanataka kumgombanisha na mashabiki wa klabu ya Yanga kwa kuibua habari ambazo hazina ukweli wowote.
"Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia, nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga," amesema Chirwa.
Kuhusu tuhuma za kugoma kusafiri na timu, Chirwa amesema nazo ni mwendelezo wa uzushi chonganishi kwa kuwa ni kweli aliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji.
"Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, huu ni upuuzi,mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hatima yangu ya baadae,niacheni nicheze mpira."
Chirwa amebaki jijini Dar es salaam kuendelea na matibabu ya maumivu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majimaji

ADVERTISE HERE