Droo ya hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho, itafanyika keshokutwa Jumatano huko Misri
Droo hiyo itafanyika saa 7 mchana, Azam Tv watarusha tukio hilo 'mbashara'
Yanga ni miongoni mwa timu 16 ambazo zitapangwa katika makundi manne ya timu nne nne kwenye kombe la Shirikisho
Yanga imewekwa katika poti ya 2 ikiwa pamoja na Motema Pembe, AS FAR, na US Monastir ambao waliwaondoa mabingwa watetezi RS Berkane
Timu ambazo ziko kwenye poti moja hazitakutana kwenye hatua ya makundi ambapo kila kundi litakuwa na timu moja kutoka kila poti
Poti ya 1 ina timu za TP Mazembe, Pyramids, Asec Mimosas na USM Alger
Yanga itapangwa kundi moja na timu yoyote kutoka poti ya 1,3 na 4




ADVERTISE HERE