Mlinzi wa kushoto wa Yanga Joyce Lomalisa Mutambala sasa anawaziba midomo wale waliokuwa wakikosoa usajili wake
Ubora alioonyesha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars ni mwendelezo wa kazi nzuri anayofanya katika kikosi cha Yanga
Lilikuwa suala la muda tu, Lomalisa kudhihirisha umahiri wake
Wakati mwingine mchezaji anapojiunga na timu mpya katika nchi nyingine huhitaji kuzoea mazingira, ligi na hata wachezaji wenzake
Changamoto iliyokuwa ikimkabili Lomalisa hakuwa ameingia katika mfumo wa kocha Nasreddine Nabi, jambo ambalo sasa amefanikiwa
Lomalisa ni mlinzi wa pembeni wa kisasa ambaye anafanya kazi ya kulinda na kushambulia
ADVERTISE HERE