Baada ya kucheza mechi tano za ligi kuu pasipo kufunga bao, jana mshambuliaji Fiston Mayele alirejea kibabe kwenye mwendo wake wa kutetema akifunga hat-trik katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mayele alishuka dimbani jana ikiwa ni siku mbili tu baada ya mkewe kujifungua mtoto wake wa tatu aliyemwita Maraelle
Mayele amesema hat-trik aliyofunga ilikuwa zawadi ya mwanawe huyo wa kike
Mayele amefikisha mabao sita sasa akihitaji kufunga bao moja tu kumfikia kinara wa mabao Sixtus Sabilo wa Mbeya City mwenye mabao saba
ADVERTISE HERE