Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amewataka Watanzania kuiombea dua klabu ya Yanga ili iweze kufuzu hatua inayofuata michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Yanga itashuka katika uwanja wa Stade Linite kesho kuivaa St Louis kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya ligi ya mabingwa.
Akizungumza leo baada ya mazoezi ya asubuhi, Nadir amesema wamejiandaa kufanya vizuri katika mchezo huo, kikubwa wanahitaji dua kutoka kwa WanaYanga wote na Watanzania kwa ujumla.
"Tunashukuru Mungu tumemaliza salama mazoezi tayari kwa mchezo wa kesho. Kila mchezaji ana hamu ya kushuka dimbani hiyo kesho, kikubwa tunaomba watanzania watuombee dua ili tuweze kufanya vizuri"
Aidha ushindi wa bao 1-0 iliyopata Yanga katika mchezo wa kwanza, Nadir amesema utawasaidia kuufanya mchezo huo uwe wa wazi zaidi.
"Ushindi wa 1-0 tulioupata nyumbani sio mdogo. Jukumu letu kubwa ni kuulinda pia kuongeza mabao zaidi"

ADVERTISE HERE