Mlinzi wa kulia wa Yanga Djuma Shabani 'Soldier ya Bemba' yuko timamu kiafya baada ya kupona majeraha ya nyama za paja yaliyomfanya akose mechi kadhaa zilizopita
Djuma amejumuishwa kwenye kikosi kilichosafiri mkoani Singida kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Liti
Nyota huyo wa zamani wa AS Vita anarejea kikosini wakati Kibwana Shomari na Joyce Lomalisa wakiwa 'wamewaka' kwelikweli
Baada ya kun'gara katika mchezo kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain, kocha mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amemtumia Lomalisa katika mechi za ligi zilizopita dhidi ya Kagera Sugar na Singida Big Stars, akimtumia Kibwana upande wa kulia
Kurejea kwa Djuma kunamuongeza ushindani kwa walinzi wa pembeni
ADVERTISE HERE