Kule Tunisia katika mchezo wa play-off kuwania kutinga makundi michuano ya kombe la Shirikisho dhidi ya Club Africain, Yanga ilitumia jezi yake ya tatu yenye rangi nyeusi
Wananchi wakapiga kandanda la kutisha ugenini na kufuzu kwenda makundi ya Shirikisho kwa kuwachapa Club Africain bao 1-0 katika uwanja wao
Yanga iliporejea kwenye ligi, kule Mwanza walipowakabili Kagera Sugar wakavaa tena uzi huo na pia wakaibuka na ushindi wa bao 1-0
Mchezo uliofuata dhidi ya Singida Big Stars, Wananchi wakaamua tena kutinga uzi huo, likapigwa 'pira' la World Cup Singida Big Stars wakachezea kipigo cha mabao 4-1 pale kwa Mkapa
Unaweza kusema jezi nyeusi ina upepo mzuri kwa Yanga kwani inaonekana kila wachezaji wanapoivaa, wanakuwa na mzuka wa kuipambania Yanga
Tusisahau jezi hii ndio imevunja rekodi ya mauzo msimu huu, kwani ndio jezi pendwa zaidi na Wananchi
Haitakuwa ajabu leo Wananchi wakiitumia tena katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa uwanja wa Liti mkoani Singida