Wakati alipocheza mechi tano mfululizo pasipo kufunga bao ndani ya ligi kuu ya NBC, kuna walioanza kumbeza mfalme wa kutikisa nyavu, Fiston kalala Mayele
Lakini Mayele ametumia mechi mbili tu, kuwafunga midomo kwani katika mechi hizo amefunga mabao matano
Mayele alifunga hat-trik katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars na jana almanusra afunge hatrik ya pili mfululizo katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji ambao aliweka kambani mabao mawili
Katika mwezi Novemba mpaka sasa Mayele amehusika kwenye mabao saba ya Yanga, amefunga matano na kutoa pasi mbili za mabao
Sasa yuko pale kileleni katika mbio za ufungaji bora akiwa na mabao nane, halafu hata haringi!
Jana baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Mayele alishangaa pale mtangazaji alipomuuliza unajisikiaje sasa ukiongoza mbio za ufungaji bora?
"Kwani mimi ndio naongoza kwenye ufungaji? hata nilikuwa sijui," alijibu Mayele