Kesho Wananchi wanarudi uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Hii inaweza kuwa moja ya mechi bora zenye ushindani katika ligi msimu huu. Ni mechi ya rekodi, mechi ya heshima na mechi ya kudhihirisha ubora
Katika mechi sita zilizopita kuzikutanisha Yanga na Mbeya City, mechi tano zilimalizika kwa sare huku Yanga ikishinda mechi moja
Wakati Yanga ikisaka rekodi ya kucheza mechi 49 pasipo kupoteza, Mbeya City watakuwa wakisaka rekodi ya kucheza mechi 10 mfululizo pasipo kupoteza msimu huu
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao huku akiahidi wataifikia rekodi ya mechi 49 pasipo kupoteza iliyowahi kuwekwa na vinara wa ligi kuu ya Uingereza, Arsenal
Baada ya ushindi dhidi ya Dodoma Jiji siku ya Jumanne, Yanga ilirejea mazoezini jana kwa baadhi ya wachezaji huku wengine wakiatarajiwa kuungana na wenzao siku ya leo kukamilisha maandalizi ya mwisho