Msuva, Singano mambo safi Difaa Al Jadida

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
17 Jul 2017
Msuva, Singano mambo safi Difaa Al Jadida
Wakati winga wa zamani wa Azam FC Ramadhani Singano 'Messi' akiwa tayari ametua nchini Morocco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida inayoshiriki ligi kuu nchini humo, winga wa Yanga Simon Msuva atajiunga na klabu hiyo baada ya mchezo wa marudiano kati ya Stars dhidi ya Rwanda, imefahamika.

Kwa muda mrefu klabu ya Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo na Difaa juu ya usajili wa mchezaji huyo.

Difaa Al Jadida imekubali kuilipa Yanga zaidi ya Mil 200 kupata sahihi ya Msuva aliyebakisha mkataba wa mwaka mmoja Jangwani.

Aidha usajili huo pia utakuwa na faida kubwa kwa Msuva mwenyewe kwani klabu hiyo imeahidi kumlipa zaidi ya Mil 150 kipindi chote cha mkataba wake pamoja na mshahara wa zaidi ya Mil 9 kwa mwezi.

Msuva amekuwa msaada mkubwa kwa Yanga katika misimu mitano iliyopita na hakika ni mmoja wa wachezaji walioitumikia Yanga kwa mapenzi makubwa.

AKiwa Difaa Al Jadida Msuva atapata nafasi ya kuonekana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa pia kama ambavyo nafasi angeipata akiwa Yanga lakini timu za Afrika Kaskazini, nyingi hufika mbali zaidi katika michuano hiyo.

Difaa ilimaliza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini Morocco.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’