Yanga ni kufa au kupona Shelisheli leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2018
Yanga ni kufa au kupona Shelisheli leo
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, Yanga leo ina kibarua kigumu mbele ya St Louis ya Shelisheli kwenye mchezo wa marudiano wa michuano hiyo hatua ya awali.

Yanga inawavaa wapinzani wao hao huku wakiwa mbele kwa bao 1-0 kufuatia ushindi walioupata kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam.

Benchi la ufundi la Yanga limesema limekiandaa kikosi chake kupata ushindi katika mchezo huo.

"Tunahitaji ushindi, ndio kitu pekee tulichokifuata huku, hautakuwa mchezo mwepesi kwa sababu kwa namna nilivyowaona wapinzani wetu, si timu ya kuidharau," amesema kocha msaidizi wa Yanga, Shedrack Nsajigwa.

Yanga leo haitakuwa na mshambuliaji wake nyota, Obrey Chirwa, lakini itawategemea nyota wengine, Ibrahim Ajibu na Papy Tshishimbi kuzamisha jahazi la St Louis.

Hafidh Saleh, Meneja wa Yanga amesema wachezaji wote waliosafiri na timu hiyo wako timamu kiafya hivyo ni uamuzi wa benchi la ufundi juu ya nani atacheza.

Kwenye mchezo wa kwanza kwenye uwanja wa taifa, goli pekee la Yanga lilifungwa na kiungo Juma Mahadhi huku pia mashabiki wakishuhudia Chirwa akikosa penalti.

Hata hivyo St Louis ilitumia mfumo wa kujihami zaidi lakini leo wanatarajiwa kucheza tofauti kwa kuwa tayari wako nyuma kwa bao 1-0.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’