Mshambuluaji wa Yanga Fiston Mayele ametoa ufafanuzi wa aina ya ushangiliaji alioutumia baada ya kufunga bao la kwanza katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City
Mayele alishangilia kama afanyavyo mshambuliaji wa Mbeya City Tariq Seif ushangiliaji ambao hutumiwa na Mbeya City wanapofunga bao
Mayele amesema wakati wa mazoezi kabla ya mechi, wachezaji wa Mbeya City walitumia aina yao ya ushangiliaji mbele ya mashabiki wa Yanga 'waliwachokoza'
"Baada ya kufunga bao langu la kwanza leo nasherehekea na timu pinzani wakicheza kwani kabla ya mchezo wakiwa katika warm up walicheza kutuchokoza na hiyo ilikuwa ni kutukosea heshima ndiyo maana nami nikacheza ngoma yao baada ya kufunga goli langu la kwanza," aliandika Mayele kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
