Kikosi cha Yanga kimewasili mkoani Mbeya usiku wa kuamkia leo kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Highland estate, Mbeya
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ametua Mbeya akiwa na kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya kuwania alama tatu dhidi ya Ihefu Fc
Wachezaji Feisal Salum na Bernard Morrison hawakujumishwa katika msafara huo wakiwa ni majeruhi
Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Erick Johora, Kibwana Shomary, Joyce Lomalisa, Davic Bryson na Dickson Job ni miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa katika msafara huo
Wengine ni nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Zawadi Mauya, Yannick Bangala, Salum Abubakar na Stephane Aziz Ki
Pia wamo Denis Nkane, Jesus Moloko, Dickson Ambundo, Clement Mzize, Fiston Mayele na Tuisila Kisinda