Kipigo cha mabao 2-1 ambacho Yanga wamekutana nacho leo huko Mbeya dhidi ya Ihefu Fc, ni cha pili kwenye ligi kwa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi
Nabi alijiunga na Yanga April 2021 na alianza kukaa kwenye benchi kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Azam Fc, April 25 2021 na Yanga kupoteza kwa kufungwa bao 1-0
Nabi alichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa kwa muda na Kocha Juma Mwambusi ambaye hii leo ameiongoza Ihefu Fc kupata ushindi dhidi ya Yanga
Pamoja na kupoteza mchezo wa leo, profesa Nabi anaendelea kubaki kama kocha bora zaidi hapa Tanzania
Amepoteza mchezo katika siku ambayo hakuna jambo angeweza kufanya, wachezaji hawakuwa katika ubora wao
Alijaribu kila aina ya mbinu na wakati mwingine kuingia kwenye mgogoro na waamuzi wasaidizi kupelekea akapewa kadi ya njano
Kiufupi ilikuwa siku mbaya ofisini...!