Mabingwa watetezi michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Yanga wanaanza kampeni ya kutetea taji hilo dhidi ya Kurugenzi Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Disemba 09-11 2022
Droo ya raundi ya pili ya michuano hiyo ambayo ilifanyika mapema leo Makao Makuu ya Azam TV ambao ndio wadhamini
Yanga walitwaa taji hilo msimu uliopita kwa kuifunga Coastal Union mikwaju ya penati 4-1 baada ya matokeo ya sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Huu ni msimu mwingine Wananchi wanataka kurudia kile walichofanya msimu uliopita kwa kushinda mataji yote ya ndani
Tayari wameweka kibindoni Ngao ya Jamii, bado taji la Ligi Kuu na hili la FA
ADVERTISE HERE