Juma Nyoso alifanya faulo mbaya sana dhidi ya Fiston Mayele jana katika moja ya matukio ya mchezo wa ligi kuu kati ya Ihefu Fc dhidi ya Yanga ambao wenyeji walishinda mabao 2-1
Hili ni tukio ambalo lilistahili Nyoso hata kupewa kadi nyekundu lakini hata onyo hakupewa
Ni tukio hilo ambalo lilimtia hasira Kocha Nasreddine Nabi na kupelekea kulumbana na mwamuzi wa akiba akihoji kwa nini mwamuzi hatoi kadi kwa rafu mbaya kama hii?
Kilichotokea kwa Nabi ni yeye kuonywa kwa kuonyeshwa kadi ya njano
Ni bahati mbaya tu siku ya jana shauku ya kuona Yanga inapoteza mchezo ilikuwa kubwa kwa wengi na ndio maana hutaona matukio mengine ya hatari yakijadiliwa
Hapa Nyosa alidhamiria kumvunja mguu Mayele lakini kilichomsaidia Mayele ni 'fitness' yake tu. Angekuwa mchezaji dhaifu angepata madhara makubwa sana