Vyombo vya habari vya Kimataifa vikiongozwa na BBC wameripoti rekodi iliyofikiwa na Yanga ya kucheza mechi 49 pasipo kupoteza kwenye ligi kuu
Lakini pia, hata Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) lilipongeza rekodi hiyo wakiitaja kuwa miongoni mwa rekodi bora zaidi zilizowekwa na klabu barani Afrika
Rekodi ya Yanga inashika namba nne nyuma ya Asec Mimosas, Esperance na APR
Leo La Liga nao wameipongeza Yanga kwa kuweka rekodi hiyo ya kucheza mechi 49 pasipo kupoteza
Kwa hakika Wananchi wana kila sababu ya kufurahia rekodi iliyowekwa na klabu yao, kwani sio jambo dogo
Ni rekodi ambayo pia imeitangaza Tanzania Kimataifa, kwani inapotajwa Yanga, basi na Tanzania lazima itajwe
ADVERTISE HERE