Pongezi Lwandamina, pongezi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2018
Pongezi Lwandamina, pongezi Yanga
Licha ya kucheza bila ya mshambuliaji wa asili, Yanga imefanikiwa kufuzu raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya St Louis.

Yanga imesonga mbele kwa faida ya ushindi wake wa bao 1-0 iliyopata nyumbani wiki iliyopita.

Kocha wa Yanga George Lwandamina anastahili pongezi kwa kuifanikisha Yanga kufuzu licha ya kuwakosa washambuliaji wake wote kutokana na majeruhi.

Ni mbinu za Lwandamina zilizofanikisha Yanga kufuzu kwenda raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambayo bingwa anaibuka na zaidi ya Bil 2.

Lwandamina alimpanga kiungo Pius Buswita kama mshambuliaji wa kati lakini akajaza viungo wengi katikati walioisaidia Yanga kukaa na mpira huku wakifanikiwa kuzima mashambulizi ya St louis.

Papi Tshishimbi aliyetumika kama namba 10 kwenye mchezo huo, wakibadilishana majukumu na Ibrahim Ajib kwa nyakati tofauti, walikuwa na kazi ya kuhakikisha wanaunganisha safu ya ushambuliaji na kiungo.

Kisha akawapa maelekezo walinzi/washambuliaji wa pembeni Kessy na Gadiel kujaza langoni kwa St Louis krosi za chinichini.

Ni krosi ya chini ya Hassani Kessy iliyozaa matunda kwenye dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza.

Said Juma Makapu na Pato Ngonyani walikuwa nguzo muhimu huku Makapu akin'gara zaidi akitokea upande wa kushoto.

Makapu aliumia kwenye kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Raphael Daudi.

Lwandamina amedhihirisha kuwa yeye ni miongoni mwa makocha bora kwani amekuwa akiiwezesha Yanga kupata matokeo katika mazingira magumu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’