Kikosi cha Yanga leo majira ya saa 1 usiku kitakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kurejea katika kasi yao baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu Fc
Kutakuwa na matukio maalum kabla ya mchezo ambapo uongozi wa Yanga umeandaa hafla ya kusherehekea rekodi ya 'unbeaten'
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema rekodi ya kucheza mechi 49 pasipo kupoteza ina heshima yake kwani sio kila timu au kila mchezaji anaweza kuifikia
Amesema kinachokwenda kufanyika ni Wananchi kusherehekea rekodi hiyo pamoja na kuwapongeza wachezaji na benchi la ufundi ambao ndio waliofanikisha
Shamrashamra hizo zinatarajiwa kuanza saa 8 mchana na zitaendelea baada ya mchezo
Akizungumza na wanahabari jana, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema kikosi chake leo kitakuwa na mabadiliko kidogo kutokana na baadhi ya wachezaji kukosekana huku wngine wakirejea
Kaze amesema Wananchi watarajie kuiona Yanga tofauti kabisa na ile waliyoishuhudia katika mchezo uliopita dhidi ya Ihefu Fc na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1