Licha ya kuchapwa mabao 2-1 na El Marreikh jana, Township Rollers kutoka Botswana imefuzu raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2.
Rollers walishinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza.
Mabingwa hao wa Botswana sasa ndio wapinzani wa Yanga kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa unaotarajiwa kupigwa kati ya March 06/07, 2018.
Mchezo wa kwanza utapigwa kwenye uwanja wa Taifa huku mchezo wa marudiano ukipigwa nchini Botswana kati ya March 16/18, 2018.

Yanga ina wiki mbili za maandalizi ya kuivaa Rollers.

ADVERTISE HERE