Kesho Jumapili Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na Kurugenzi Fc katika mchezo wa raundi ya pili kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Kurugenzi Fc inatokea mkoani Simiyu, msimu huu inashiriki ligi daraja la pili (first division). Yawezekana ni timu isiyo na jina kubwa lakini sio ngeni kwani ilianzishwa miaka ya 80 ikimilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mwaswa
Huu ni msimu wa pili Kurugenzi Fc kucheza ASFC msimu uliopita iliishia 16 bora, ikitolewa na KMC kwa mabao 5-2, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Timu hiyo ilitinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Kitayosce na sasa inakutana na Yanga kwa mara ya kwanza katika hatua ya 64,
Yanga ikiwa bingwa mtetezi wa michuano hii, inayo kila sababu ya kushinda hasa ikizingatiwa itacheza katika uwanja wake wa nyumbani, Benjamin Mkapa
Lakini Wananchi hawapaswi kuwadharau wapinzani wao kwani kwao kucheza na Yanga ni nafasi adimu ambayo wameipata kama bahati