Tusimpe presha Mzize - Kaze

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Dec 2022
Tusimpe presha Mzize - Kaze

Kocha Msaizidi wa Yanga Cedric Kaze amempongeza mshambuliaji kinda Clement Mzize kwa kufunga mabao manne kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Kurugenzi Fc ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana

Hata hivyo Kaze amesema Mzize hapaswi kuwekwa katika presha ya kufananishwa na wachezaji wengine kwani yeye bado anaendelea kukua

"Nimefurahi kuona amefunga mabao manne, Mzize ni mchezaji mzuri ambaye anaendelea kukua, tuendelee kumsaidia ili aweze kufikia kiwango cha juu"

"Ni mshambuliaji anayeweza kukupa vitu vingi, iwe kusimama kama mshambuliaji pekee, kushambulia kutokea pembeni, ana kasi, mbinu na uwezo mkubwa wa kufunga"

"Hata hivyo sio muda wa kumuweka kwenye presha ya kumfananisha na Mayele (Fiston), yeye bado mdogo na anaendelea kuimarika. Naamini kwa mwenendo wake, sio muda mrefu Mzize atakuwa mshambuliaji mkubwa hapa Tanzania," alisema Kaze

Pamoja na kufunga mabao manne kwenye kombe la FA, Mzize pia ana bao moja kwenye ligi kuu ya NBC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’