Kocha Sebastian Nkoma ameanza vyema majukumu yake ya kuinoa Yanga Princess baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mkwawa Queens katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake uliopigwa uwanja wa Uhuru
Precious, Wogu, Aniela na Blessing ndio waliofanikisha ushindi huo ingawa nafasi walizopoteza zilikuwa nyingi zaidi

Ni matokeo muhimu kwa Yanga Princess ambayo ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Fountain Gate Princess
Kwa kocha Nkoma ni mwanzo mzuri kwani pamoja na kuwa na timu kwa muda mfupi, mabadiliko yameonekana
Yanga Princess imemiliki mpira kwa kiasi kikubwa kulinganisha na walivyocheza mechi ya kwanza dhidi ya Fountain Gate Princes
ADVERTISE HERE