Jumamosi ya wiki hii, Disemba 17 2022, Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Utakuwa mchezo wa kwanza katika mzunguuko wa pili, ikiwa ni mechi ya 16
Katika duru hii ya lala salama, Yanga imepania kukusanya alama tatu katika kila mchezo wakianza na maafande wa Polisi Tanzania
Viingilio vya mchezo huo vimetangazwa mapema ambapo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Mchezo utapigwa kuanzia saa 1 usiku

ADVERTISE HERE