Kiungo fundi wa Yanga Salum Abubakar 'Sureboy' ni miongoni mwa wachezaji wanaojifua kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Sureboy amekuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa akiuguza majeraha, baada ya kuanza mazoezi ni wazi yuko tayari kurejea kikosini

Yanga inajifua Avic Town, Kigamboni tayari kuwakabili maafande wa Polisi Tanzania ambao wameshatua jijini Dar es salaam
Utakuwa mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Mwinyi Zahera kukabiliana na waajiri wake hao wa zamani
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua tiketi zao mapema ili kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi siku ya kesho katika mchezo wa kwanza raundi ya lala salama
ADVERTISE HERE