Klabu ya Yanga imethibitisha kumpa likizo ya mwezi mmoja mkufunzi wa magolikipa Milton Nienov raia wa Brazil
Taarifa iliyotolewa na Yanga na kuthibitishwa na Mtendaji Mkuu Andre Ntime, imebainisha kuwa Nienov aliomba arejee Brazil kwenda kushughulikia matatizo ya kifamilia na atarudi nchini Januari 16 kuendelea na majukumu yake
"Tumempa likizo ya mwezi mmoja kocha wetu Milton akashughulikie matatizo ya familia yake. Tunatarajia atarejea nchini Januari 16, 2023 kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake," alisema Ntine
Nienov atakosa mechi tatu za ligi kuu kuhitimisha mwaka 2022 pamoja na michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo itaanza Januari 1 2023 visiwani Zanzibar
ADVERTISE HERE