Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele anaendelea kuongoza katika mbio za kuwania ufungaji bora katika ligi kuu ya NBC akiwa na mabao 11 baada ya mechi za raundi ya 16
Moses Phiri wa Simba anamfuatia kwa ukaribu akiwa amefunga mabao 10
Huu unaweza kuwa msimu mzuri kwa Mayele katika dhamira yake ya kuwa mfungaji bora
Katika mechi 16, ameweza kufunga mabao 11, bado kuna mechi 14 kuhitimisha msimu huu
Msimu uliopita Mayele alifunga mabao 16 katika mechi 30, msimu huu amekuwa na uwiano mzuri zaidi
Mchezo unaofuata ni kesho Jumanne dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mayele atakuwa na nafasi nyingine ya kujiimarisha katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu

ADVERTISE HERE