Mnakumbuka ile simu ambayo mshambuliaji Fiston Mayele alipiga kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania akipachika moja ya mabao katika ushindi wa 3-0? Basi mpaka leo simu ile haijajibiwa!
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union ambao Mayele aliweka kambani mabao mawili, waliamua kumuandikia email kumkumbusha yule jamaa mbona haleti majibu?
Mayele ni mshambuliaji anayependa ushindani! msimu uliopita alifurahia 'battle' yake na George Mpole ambaye ametimka Geita Gold na kujiunga na Fc Lupopo ya DR Congo
Mayele ameendelea kukaa kileleni peke yake katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa na mabao 13
Akiwa ametajwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa DR Congo kwa mwaka 2022, siku ya Jumapili Mayele atakuwa na nafasi nyingine ya kuendelea kuongeza idadi ya mabao yake katika mchezo dhidi ya Azam Fc
Anahitaji kufunga mabao matatu tu kutoka mechi 13 zilizobaki ili kufikia rekodi yake ya mabao 16 aliyofunga msimu uliopita
Ni wazi ataivunja rekodi hiyo na kuweka rekodi nyingine mpya