Bao alilofunga katika mchezo dhidi ya Azam Fc, limefanya mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele afikishe mabao 14 katika ligi kuu ya NBC
Mayele anaikaribia rekodi yake ya mabao 16 aliyofunga msimu uliopita
Mechi 12 zimesalia kuhitimisha msimu huu, kama hatakumbana na changamoto ya aina yoyote ambayo itamuweka nje, ni wazi ana nafasi kubwa ya kuvunja rekodi yake
Mayele anaongoza mbio za ufungaji bora na mabao yake 14 akifuatiwa na Moses Phiri wa Simba mwenye mabao 10
Sixtus Sabilo ameendelea kubaki na mabao yake saba kama ilivyo kwa Idriss Mbombo wa Azam Fc
Mayele amepania kuibuka mfungaji bora msimu huu baada ya kuikosa tuzo hiyo msimu uliopita akizidiwa bao moja na George Mpole aliyefunga mabao 17
ADVERTISE HERE