Kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa kijamii, Waziri wa Fedha Mh Dk Mwigulu Nchemba ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini klabu ya Yanga, ameweka chapisho akiwa na familia yake nyumbani wakipata mlo wa sikukuu katika siku hii ya kufungua mabox ya zawadi
Kuna habari njema kwa Wananchi kwenye chapisho hilo kuhusu kiungo wao Feisal Salum 'Fei Toto'. Mh Mwigulu amedokeza kufanya mazungumzo nae
Kwa wasiofahamu Dk Mwigulu ndiye aliyemtoa Feisal visiwani Zanzibar kumleta Bara na kumsajili katika iliyokuwa klabu yake ya Singida United hata hivyo baadae akaamua kumtoa na kumpeleka Yanga
Dk Mwigulu ni miongoni mwa waliofanya jitihada kuhakikisha Fei Toto hapotoshwi kwani bado anastahili kuendelea kuitumikia Yanga!
ADVERTISE HERE