Arafat afunguka mkakati wa Yanga dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Dec 2022
Arafat afunguka mkakati wa Yanga dirisha dogo

Makamu wa Rais klabu ya Yanga Arafat Haji amewatoa hofu Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuwa watasajili wachezaji bora katika dirisha hili la usajili kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la Ufundi

Siku 11 zimepita tangu dirisha dogo la usajili lilipofunguliwa Mashabiki wakiwa na shauku ya kuona nyota wapya wakitua Jangwani kwa ajili ya kuboresha maeneo yenye changamoto

Arafat amesema tayari klabu iko kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji akibainisha kuwa watasajili wachezaji wawili au watatu

"Si tuko vizuri nawaambia Wananchi wasiwe na wasiwasi, tuko kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji. Tunaweza kusajili wachezaji wawili au watatu kabla dirisha kufungiwa"

"Pia tunao wachezaji ambao hatukuwasajili katika dirisha lililopita sasa wako tayari kuitumikia Yanga. Dhamira yetu ni kufanya maboresho ambayo yataimarisha zaidi kikosi chetu," alisema Arafat

Kulingana na mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi, mahitaji ya Yanga ni beki wa kati, kiungo mkabaji na mshambuliaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’