Jumamosi Disemba 31 2022 Yanga itakuwa kule Manungu mkoani Morogogo kuwakabili wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu, raundi ya 19
Huu ndio mchezo wa mwisho kwa mwaka 2022 Yanga ikiwa na uhakika wa kufunga mwaka 2022 ikiwa inaongoza ligi pasipo kujali matokeo ya mchezo huo
Wananchi wana alama 47 wakati Simba inayoshika nafasi ya pili ina alama 41 huku wauza ukwaju Azam Fc wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama 37
Ushindi kwa Yanga itaihakikishia Yanga kufunga mwaka 2022 ikiwa na alama 50 kileleni mwa msimamo wa ligi kama walivyofunga mwaka 2021 na alama 51
Mwaka jana Yanga iliichapa Dodoma Jiji mabao 4-0 katika mchezo wa mwisho wa kufunga mwaka
Safari hii ni zamu ya Mtibwa Sugar...!
ADVERTISE HERE