Kikosi cha Yanga knatarajiwa kuondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kufunga mwaka ligi kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Disemba 31 katika uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema timu itaondoka mchana wa leo kwenda Morogoro kupigania alama tatu muhimu ambazo zitawapa furaha Wananchi na kufunga mwaka vizuri
"Asubuhi tutakuwa na program za mazoezi kama kawaida, wachezaji watapata mlo wa mchana kabisa kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Morogoro"
"Baada ya kuhakikisha mashabiki wetu wanasherehekea vyema Christmas kwa ushindi dhidi ya Azam Fc, tunakwenda Morogoro kupigania alama tatu muhimu ambazo zitawafanya wafunge mwaka wakiwa na furaha," alisema Kamwe