Buriani mfalme Pele

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Dec 2022
Buriani mfalme Pele

Gwiji wa soka kutoka Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amefariki dunia usiku wa jana Alhamisi akiwa na umri wa miaka 82

Mtoto wake wa kike Kely Nascimento, alithibitisha kifo cha baba yake baada ya kuugua saratani ya utumbo mpana na kulazwa hospitalini ambako alikuwa akipata matibabu.

Pele ambaye alitajwa kama mchezaji bora wa karne ya 21, enzi za uchezaji wake alifanikiwa kushinda mataji matatu ya Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Brazil.

Pele ndiye mfungaji bora wa timu ya taifa ya Brazil akiwa na mabao 77 katika michezo 92 akilingana idadi hiyo ya magoli na Neymar Jr.

Katika ngazi ya klabu, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Santos ya Brazil akiwa na mabao 643 katika michezo 659.

Katika enzi ya dhahabu kwa Santos, aliiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa bara la Amerika ya Kusini maarufu kama Copa Libertadores mwaka 1962 na 1963 pamoja na klabu bingwa ya dunia enzi hizo ikiitwa Kombe la Mabara mwaka 1962 na 1963.

Anatajwa kama mchezaji aliyefunga zaidi ya magoli 1000 kwenye maisha yake ya soka

Dunia inaomboleza kifo cha gwiji huyu ambaye historia yake itahadithiwa kwa vizazi na vizazi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
16h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
20h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
21h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
21h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’