Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amefichua siri ya mashuti ya kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye leo amefunga bao pekee la Yanga katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Kaze amesema umahiri wa Aziz Ki kupiga mipira ya adhabu unatokana na mazoezi ambayo huwa anafanya
"Azizi Ki hufanya mazoezi binafsi ya kupiga mipira ya adhabu kila tukimaliza mazoezi ya timu. Kwa kawaida hupiga mashuti 20-25 katika maeneo mbalimbali"
"Pamoja na ubunifu wake sisi tunampa maelekezo madogo madogo ili kuona ana ufanisi zaidi," alisema
Aziz Ki amewaachia msala walinda lango wa timu mbalimbali za ligi kuu ambao wameendelea 'kutaabika' na mashuti yake
ADVERTISE HERE