Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ametangazwa kuwa mchezaji bora wa DR Congo kwa mwaka 2022
Mayele ameshinda tuzo hiyo ikiwa moja ya tuzo za LLF Awards ambazo hutolewa kila mwaka na mtandano wa Leopard Leader
Mayele amepata asilimia 81 ya kura zote zilizopigwa, kwa mara nyingine Wananchi wakihakikisha anashinda tuzo hiyo
Ukizungumzia mshambuliaji wa Ki-Congo aliyefanya vizuri zaidi miongoni mwa wanaocheza Afrika na hata huko Ulaya, hakuna aliyemzidi Mayele
Msimu uliopita Mayele alifunga mabao 18 katika mashindano yote wakati msimu huu amepachika mabao 23 katika mashindano yote
Katika msimu mmoja na nusu akiwa na Yanga, Mayele amefunga mabao 30 kwenye ligi pekee
ADVERTISE HERE