Wachezaji wengi wa Kizanzibar ambao wamepata nafasi kucheza soka Tanzania Bara, waliotamba zaidi ni wale walioitumikia Yanga
Rudi nyuma kabisa enzi za akina Abdi Kassim, Nadir Haroub 'Cannavaro' na hata Feisal Salum 'Fei Toto'
Mudathir Yahya ni miongoni mwa wachezaji kutoka visiwani ambapo wametengneza majina Bara lakini sio wachezaji waliozungumzwa sana
Katika misimu ambayo Mudathir aliitumikia Azam Fc alikuwa katika kiwango bora sana, kama wakati huo angekuwa Yanga pengine jina lake lingezungumzwa zaidi ya Fei Toto
Mudathir amejiunga na Yanga wakati sahihi, huu ndio wakati wake Watanzania kumtambua sasa kwa kuwa amejiunga na timu kubwa
Huyu ni kiungo ambaye amezitumikia timu za Taifa za 'Stars' na Zanzibar Heroes kwa mafanikio
Ni usajili ambao unaweza usizungumzwe sana, lakini wale wenye mashaka wasubiri kuona majibu yake uwanjani
