Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga leo wanaanza kampeni ya kuwania taji la Mapinduzi watakaposhuka uwanja wa Amaan kupepetana na KMKM katika mchezo utakaopigwa saa 2:15 usiku
Ni mchezo muhimu kwa Yanga kupata ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali
Singida BS walishinda mabao 2-0 walipokutana na KMKM hivyo Yanga inahitaji ushindi pia kabla ya mchezo wao dhidi ya Singida BS
Jana watani zao Simba waliondoshwa mapema kwenye michuano hiyo baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mlandege
Katika mchezo huo, Yanga inatarajiwa kuwatumia nyota wake Lazarus Kambole, Yacouba Songne na Mudathir Yahya ambaye alitua visiwani Zanzibar mapema jana baada ya kukamilisha usajili wake na Yanga

ADVERTISE HERE