Bao la dakika ya 95 lililofungwa na Dickson Ambundo limetosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya KMKM
Ulikuwa ni mchezo ambao ulionekana kama ungemalizika kwa matokeo ya suluhu kabla ya nafasi muhimu waliyoipata Yanga kwenye dakika ya 95
Kwa mara ya kwanza leo Yanga imewatumia Lazarus Kambole na Yacouba Songne ambapo Yacouba aliingia dakika 15 za mwisho sambamba na Mudathir Yahya na kuongeza kasi ya mashambulizi ya Yanga
Ushindi huo unaweka hai matumaini ya Yanga kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi lakini itahitaji ushindi dhidi ya Singida BS
ADVERTISE HERE