Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa mchezaji mmoja katika dirisha hili dogo ambalo litafungwa Januari 15 2023
Mudathir Yahya alitambulishwa kujiunga na Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na Azam Fc
Hata hivyo Yanga bado haijafunga usajili, kwani kuna majembe mengine mawili yanasubiri kutambulishwa
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewahakikishia Wananchama na Mashabiki wa timu hiyo kuwa ndani ya siku hizi chache zilizosalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa kuna usajili 'mzito' utatambulishwa
Arafat amesema usajili huo umezingatia mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Nasreddine Nabi
ADVERTISE HERE