Kikosi cha Yanga kilirejea Dar kutoka visiwani Zanzibar jana ambako walishiriki michuano ya kombe la Mapinduzi
Yanga inaelekeza nguvu kwenye mashindano yaliyo mbele ambapo wiki ijayo, Januari 16 watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ihefu Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Kikosi kinatarajiwa kurejea mazoezini kesho Jumatatu kuanza maandalizi ya mchezo huo
Wakati timu ikirejea mazoezini, mashabiki wa Yanga bado wana shauku ya kufahamu timu yao inafungaje dirisha dogo la usajili
Kuna siku saba zimebaki kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 15 2023
Ahadi iliyotolewa ni kuwa, bado kuna utambulisho wa wachezaji wawili wa kigeni ambao utafanyika kabla ya dirisha kufungwa
ADVERTISE HERE