Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amekipongeza kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi licha ya kushindwa kutinga hatua ya nusu fainali
Baada ya kipigo cha mabao 4-1 ambacho Azam Fc wamekumbana nacho dhidi ya Singida BS hapo jana, Kamwe amesema matokeo hayo yanadhihirisha ubora wa timu yao iliyoshiriki Mapinduzi Cup ukilinganisha na timu nyingine ambazo zilipeleka vikosi vyao vya kwanza kushiriki michuano hiyo
"Mashabiki na Wanachama wa Yanga tunatakiwa tujivunie sana ukubwa na ubora wa kikosi chetu. Hii timu haikufungwa mchezo wowote Mapinduzi Cup 2023"
"Ilimaliza Kundi B ikilingana pointi na Singida Big Stars Kilichowahukumu ni Goal Difference Tu. Achana na hilo, njoo kwenye Performance. TOP KABISA. Sio KMKM wala Singida Big Stars waliomaliza Dakika 90 kirahisi. Walipigiwa mpira mkubwa mno"
"Kilichotokea jana, kimethibitisha kuwa YANGA TUNAWEZA KUWA NA TIMU 2 BORA kwenye Ligi ya NBC na zote zikashindania ubingwa," alitamba Kamwe
Kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi kilijumuisha wachezaji 13 wa timu ya wakubwa na wachezaji 12 wa timu ya vijana
Katika michuano hiyo Yanga iliwapa nafasi wachezaji ambao hawakutumika sana kwenye ligi na mashindano mengine