Kumekuwa na mjadala mkali miongoni mwa mashabiki wa Yanga juu ya mlinda lango gani anastahili kulinda lango la Yanga kwa wakati huu.
Mcameroon Youthe Rostand amekuwa chaguo la kwanza tangu mwanzoni mwa msimu huu lakini siku za hivi karibuni ameonekana kufanya makosa hasa katika kufanya maamuzi anapotokea krosi.
Bao alilofungwa dhidi ya St Louis siku chache zilizopita linafanana kabisa na bao alilofungwa na Jaffar Mohammed kwenye mchezo dhidi ya Majimaji leo.

Wakati alipokuwa majeruhi, kinda Ramadhani Kabwili alipata nafasi ya kudaka michezo kadhaa. Kinda huyo pia alifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu.
Kiwango chake kiliwavutia wengi.
Benno Kakolanya hajawa na msimu mzuri kutokana na kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara pamoja na kuwa na matatizo binafsi na uongozi wa Yanga mpaka kupelekea akafanya migomo 'baridi'

Jambo la msingi hapa ni kwamba walinda lango wote wa Yanga wana viwango vizuri kila mmoja anakuwa na mapungufu yake, ni kawaida.
Kocha wa makipa Juma Pondamali aliwahi kufunguka juu ya malalamiko ya baadhi ya WanaYanga kuhusu makosa ya Rostand na alisema amekuwa akiyarekebisha.
Kuna kipindi Rostand alikuwa akilalamikiwa juu ya uwezo wake katika kuzuia changamoto ya mikwaju ya penati.
Moja ya kazi kubwa aliyoifanya Rostand baada ya malalamiko yale ni kufanyia kazi udhaifu wake katika kuzuia matuta.
Matunda yake aliivusha Yanga kwenye mchezo dhidi ya Ihefu kwa kuzuia mikwaju mitatu.
Muhimu ni kuendelea kumuunga mkono Rostand na wenzie na kuwatia moyo ili waendelee kujituma na kujisahihisha pale wanapokosea.
Hakuna mlinda lango aliyekamilika kwa asilimia 100%, hasa linapokuja swala la kucheza krosi na mipira ya chini. Huu ni ugonjwa wa makipa wengi duniani.

ADVERTISE HERE